12. Mfano wa saba kuonyesha jinsi Raafidhwah wanavodai kuwa Maswahabah wamepotosha Qur-aan

al-Kulayniy amesema katika “al-Kaafiy”:

“Wengi katika watu wetu waaminifu wameeleza kutoka kwa Ahmad bin Muhammad, kutoka kwa al-Hajjaaj, kutoka kwa ´Aliy bin ´Uqbah, kutoka kwa Daawuud bin Firqab kutoka kwa yule aliyepokea kutoka kwa Abu ´Abdillaah ambaye amesema:

“Qur-aan imeteremshwa ikiwa robo nne (1/4); moja ni kuhusu halali, nyingine ni kuhusu haramu, nyingine ni kuhusu mifano na hukumu, nyingine inahusu yaliyopitika kabla yenu, yatayopitika baada yenu na utawala kati yenu.”[1]

Iko wapi sehemu ya watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Vipi kuhusu maadui zao? Vipi kuhusu kufufuliwa na kulipwa? Vipi tutatue tofauti hii ya wazi baina ya kauli ya ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu) na kauli ya Abu ´Abdillaah? Tunachoweza kusema tu ni kwamba Allaah Amewatakasa watu wawili hawa na uongo na uzushi huu.

[1] 02/627.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 41
  • Imechapishwa: 19/03/2017