12. Mahari yanatakiwa kutolewa yote kikamilifu

Miongoni mwa haki za wanandoa wakati wa kufunga ndoa ni mwanaume ampe mwanamke mahari yake yote kikamilifu. Yasipunguzwe. Yatolewe kama jinsi wanandoa walivyokubaliana. Allaah (Ta´ala) Amesema:

وَآتُوا النِّسَاءَ صَدُقَاتِهِنَّ نِحْلَةً

“Na wapeni wanawake mahari zao kwa maridhawa.”[1]

Amesema (Ta´ala) vilevile:

وَإِنْ أَرَدتُّمُ اسْتِبْدَالَ زَوْجٍ مَّكَانَ زَوْجٍ وَآتَيْتُمْ إِحْدَاهُنَّ قِنطَارًا فَلَا تَأْخُذُوا مِنْهُ شَيْئًا

“Na mkitaka kubadlisha mke mahali pa mke, na mmempa mmoja wao [zawadi ya] mirundi ya mali, basi msichukue humo chochote.”[2]

[2] 04:20

[2] 04:04

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 19
  • Imechapishwa: 24/03/2017