12. Mafungamano ya al-Albaaniy na Juhaymaan al-´Utaybiy


Mtu huyu ameitakasa tuhuma yake dhidi yake kwamba ana tamaa ya kisiasa kwa kuifungamanisha na harakati zinazodaiwa kwamba ni za al-Mahdiy kwa Shaykh al-Albaaniy[1]. Hapana shaka kwamba zile harakati zinazoitwa kwamba ni za al-Mahdiy zilizokuwa katika karne ya kumi na tano ni za kidhulma na mbaya. Waliushambulia msikiti Mtakatifu na wakawaua waswaliji sehemu hiyo. Wahalifu hao walijiwajibishia matishio makali. Walimwaga damu ya wasiokuwa na hatia na wakawaua watu wasiokuwa na makosa. Wakajivua katika utawala wa mtawala wa Kiislamu katika msikiti Mtakatifu. Hivyo wakawa ni wenye kustahiki matokeo yote yanayopelekea katika hayo. Allaah aliwashinda na wakapata malipo yao hapa duniani. Tunafikiria kuwa watakuwa na hali nzito kabisa mbele ya Allaah siku ya Qiyaamah. Kadhalika kumtuhumu Shaykh al-Albaaniy kwa kitu kama hicho cha madhambi kilichotokea pasi na dalili ya wazi ni jambo la khatari. Mbele ya Allaah dhambi hiyo ni nzito zaidi.

Ikiwa mtu atasema kwamba baadhi yao walikuwa ni katika wanafunzi zake, mwalimu habebi jukumu la kosa la mwanafunzi. Waaswil bin ´Atwaa´ na ´Amr bin ´Ubayd wote wawili walitoka katika masomo ya al-Hasan al-Baswriy. Hawa wawili ndio walioasisi ´Aqiydah ya Mu´tazilah. Hakuna yeyote katika Salaf aliyemtia kasoro al-Hasan al-Baswriy juu ya matendo yao. Hakuna ambaye alidai kwamba ni washirika wake. Heshima ya muislamu haitakiwi kuchafuliwa pasi na dalili ya wazi, khaswakhaswa wanachuoni ambao wameutumikia Uislamu na waislamu kwa kiasi kikubwa.

[1] Uk. 21

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fath ar-Rabbaaniy fiyd-Difaa´ ´an-ish-Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy, uk. 31-33
  • Imechapishwa: 17/11/2018