12. Madhehebu ya Murji-ah


2- Kundi la pili: Murji-ah ambao wanasema imani iko ndani ya moyo na wala ndani yake hakuingii matendo. Baadhi yao wanasema ndani ya imani hakuingii maneno. Wanaonelea kuwa imani iko moyoni tu. Kuhusu matendo hayaingii. Mtu akifanya yakufanya basi hakufuru na wanasema:

“Maasi pamoja na imani hayadhuru kama ambavyo kufuru pamoja na utiifu haunufaishi kitu.”

Huu ndio msingi wao. Wametendea kazi maandiko ya ahadi ambapo Allaah kaahidi msamaha na rehema na wakati huohuo hawakutendea kazi maandiko ya matishio na wakategemea juu ya matarajio pekee. Upande mwingine Khawaarij wamatendea kazi maandiko ya matishio na wakaacha kutendea kazi maandiko ya ahadi, rehema na kutubu. Wameegemea zaidi upande wa khofu na wakawa na khofu kubwa na wakaegemea zaidi upande wa kuwakufurisha watu na kuhalalisha damu na mali zao kutokana na madheheb yao yaliyoharibika.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 26
  • Imechapishwa: 06/05/2018