12- Madhambi yanapelekea mtu kuyaona ya kawaida


Madhambi yanapelekea kuufanya moyo kuyaona kuwa ni mabaya. Yanakuwa kwake kama jambo la kawaida. Mwishowe anakuwa haoni haya tena kwa watu kumuona akitenda dhambi na kumtukana kwayo. Haya ni katika kile kilele cha kutokuwa na aibu na ni ladha kwa wale mabingwa wa kutenda madhambi. Baada ya hapo wanaanza kujifakhari kati yao na wanawaeleza kwayo wale ambao hawakujua kuwa waliyatenda. Sampuli hii ya watu hawatosamehewa. Mara nyingi njia ya kuiendea tawbah huwa ni yenye kufungwa kwao. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ummah wangu wote ni wenye kusamehewa isipokuwa wale wenye kufanya madhambi hadharani. Katika kudhihirisha ni Allaah kumsitiri mja kisha anaamka asubuhi na kuanza kuifichua nafsi yake na kusema: “Ee fulani! Nilifanya hivi na hivi siku fulani.” Anaifedhehesha nafsi yake baada ya kuwa Mola wake amemsitiri usiku.”[1]

[1] al-Bukhaariy (6069) na Muslim (2990).

  • Mhusika: Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Daa’ wad-Dawaa’, uk. 69