Kuhusu kuamini misingi mingine ya dini ni kuamini Malaika, Vitabu Vyake, Mitume Yake, siku ya Mwisho na kuamini Qadar kheri na shari yake. Yote haya yanafuata baada ya kumuamini Allaah (´Azza wa Jall). Vilevile yote haya ni matawi ya kumuamini (Subhaanahu wa Ta´ala). Ametukhabaisha kuwepo kwa Malaika na mambo yaliyopita, kuhusu kutumwa kwa Mitume, siku ya Mwisho na yatayopitika ndani yake. Kwa hivyo ni wajibu kwetu kuamini hayo. Mengi katika hayo yanahusiana na kuamini mambo yaliyofichikana.

Sisi tunamuamini Allaah na Malaika Wake. Haya ndio mambo makubwa katika kuamini mambo yaliyofichikana.

Vilevile tunawaamini Mitume hata kama hatukuwaona. Hata hivyo tunawaamini kwa kuwa Allaah (´Azza wa Jall) ndiye katujuza hayo. Ametukhabarisha kwamba amewatuma Mitume ambao wamekuja kutoa biashara njema na kuonya.

Mtume wa kwanza ni Nuuh na wa mwisho ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhimaa wa sallam).

Vivyo hivyo tunawaamini Malaika ijapo hatujawaona. Hata hivyo tunawaamini kwa kuwa Allaah (´Azza wa Jall) na Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio wametujuza hayo.

Tunaamini pia siku ya Mwisho ingawa bado haijafika. Hata hivyo kwa hayo tunategemea maelezo ya Allaah na Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hiyo ndio imani sahihi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mujmal ´Aqiydat-is-Salaf as-Swaalih, uk. 12
  • Imechapishwa: 24/05/2022