12. Inafaa kwa msafiri asiyefunga kujumuisha Swalah?

Swali 12: Nikiwa msafiri asiyefunga inajuzu kwangu kujumuisha swalah au msafiri tu ndiye anaweza kufanya hivo?

Jibu: Kujumuisha kati ya swalah mbili haikushurutishwa kufunga. Kama msafiri inajuzu kwako kuacha kufunga na kujumuisha swalah.

Maoni sahihi ni kwamba inajuzu kufunga na kuacha kufunga katika safari. Lakini lililo bora ni kuacha kufunga kwa kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anapenda zichukuliwe ruhusa Zake kama anavyochukia kuasiwa[1].

[1] Ahmad (832). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ul-Jaami´” (1886).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 27
  • Imechapishwa: 12/06/2017