Wakamwamini Allaah hali ya kuwa ni wenye kutamka kwa ndimi zao na wenye kumtakasia nia kwa nyoyo zao. Wakatendea kazi yale waliyoletewa na Mitume Yake na kufikishwa na Vitabu Vyake… – Hii ndio natija ya uongofu wa maelekezo; wameikubaki haki kwa kutamka na kuamini moyoni. Haitoshi peke yake kutamka kwa mdomo. Aidha ni lazima kutamka kwa mdomo mtu pia aamini ndani ya moyo. Wanafiki ndio hutamka kwa mdomo pasi na kuamini ndani ya moyo. Waumini wao wanaikubali haki kwa kutamka kwa mdomo na kutakasa nia kwa nyoyo zao. Haki ni lazima ikubaliwe kwa kutamka kwa mdomo na kutakasa nia kwa nyoyo. Kusiweko jambo la kujionyesha wala kutaka kukisika, jambo la kujifanya wala unafiki.

Utamke kwa mdomo wako, usadikishe kwa moyo wako na ufanye matendo kwa viungo. Huu ndio uhakika wa imani tofauti na Murji-ah katika madhehebu yao potofu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 16-17
  • Imechapishwa: 05/07/2021