3- Inafaa kwa mgonjwa kula mchana wa Ramadhaan na alipe zile siku alizokula. Vivyo hivyo mwanamke mwenye mimba na mnyonyeshaji pindi watapochelea juu ya nafsi zao au watoto wao. Hapo wana ruhusa ya kula na walipe. Kwa sababu wana huku moja kama mgonjwa. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“Atakayekuwa mgonjwa au safarini basi atimize idadi katika siku nyinginezo.”[1]

Maradhi yenye kujuzisha kuacha kufunga ni yale makubwa yenye kuzidi kwa kufunga au mtu anachelea yakachelewa kupona[2].

Wanachuoni wameafikiana juu ya kufaa mgonjwa kuacha kufunga kwa ujumla. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ

“Hakukufanyieni ugumu wowote ule katika dini.”[3]

Tofauti na maradhi mepesi ambayo hali inaweza kuwa ngumu kidogo kwa mgonjwa akifunga lakini hayaiathiri swawm. Maradhi kama haya hayamjuzishii mtu kula. Bali italazimika kwake kufunga kwa sababu anaingia ndani ya ujumla wa maneno Yake (Ta´ala):

فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ

“Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi mpya na afunge.”[4]

[1] 02:185

[2] Tazama ”al-Mughniy” (03/1155) ya Ibn Qudaamah.

[3] 22:78

[4] 02:185

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtaswaru fiy Ahkaam-is-Swiyaam, uk. 18
  • Imechapishwa: 23/05/2019