735- Muhammad bin ´Abdir-Rahmaan bin Zuraarah amesema: “Nimemsikia ami yangu[1], ambaye hatujapatapo kuona mtu anayefanana naye, akisimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule atakayesikia wito siku ya ijumaa na asiuendee, kisha akausikia na asiuendee, kisha akausikia na asiuendee, basi Allaah atapiga muhuri juu ya moyo wake na ataufanya moyo wake kuwa moyo wa mnafiki.”

Ameipokea al-Bayhaqiy.

[1] Jina la ami yake ni Yahyaa bin Sa´d bin Zuraarah. Hivyo basi itakuwa Abu Ya´laa ameipokea katika ”al-Musnad”. Ilikuwa inasilihi zaidi kuiegemeza kwake kuliko kwa al-Bayhaqiy ambaye ameipokea katika ”ash-Shu´ab” (3/102-103).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/453)
  • Imechapishwa: 26/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy