12. Hadiyth “Miongoni mwa wakweli na mashahidi… “


1003- ´Amr bin Murrah al-Juhaniy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Kuna mtu alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Unaonaje lau nitashuhudia ya kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na kwamba wewe ni Mtume wa Allaah, nikaswali swalah tano, nikatoa zakaah, nikafunga Ramadhaan na nikafanya ´ibaadah juu ya nyusiku zake. Nitakuwa katika watu sampuli gani?” Akasema: “Miongoni mwa wakweli na mashahidi.”

Ameipokea al-Bazzaar, Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” na Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh”. Tamko ni la Ibn Hibbaan.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/587)
  • Imechapishwa: 26/05/2018
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy