60- ´Amr bin Zaraarah amesema:

“Wakati nilipokuwa nimesimama na napiga visa ´Abdullaah (bi maana Ibn Mas´uud) alisimama mbele yangu akasema: “Ee ´Amr! Hakika wewe ima umezusha Bid´ah potevu au umeongozwa zaidi kuliko Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake.” Niliona namna watu walivyokimbia mbali nami mpaka nikajiona nimebaki peke yangu.”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika “ ”al-Mu´jam al-Kabiyr”  kwa cheni mbili ambapo moja katika hizo ni Swahiyh[2].

[1] Swahiyh kupitia zengine.

[2] ad-Daarimiy amepokea mfano wake ambayo ni timilifu zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/132)
  • Imechapishwa: 27/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy