12. Hadiyth “Atakayefunga siku moja katika njia ya Allaah, Allaah atautenga mbali… “

989- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayefunga siku moja katika njia ya Allaah, Allaah atautenga mbali uso wake na Moto kwa ajili ya siku hiyo miaka sabini.”[1]

Ameipokea an-Nasaa´iy kwa cheni ya wapokezi nzuri na at-Tirmidhiy kupitia kwa Lahiy´ah- at-Tirmidhiy amesema:

“Hadiyth geni.”

Imepokelewa vilevile na Ibn Maajah kupitia kwa ´Abdullaah bin ´Abdil-´Aziyz al-Laythiy. Cheni ya wapokezi iliyobaki ni waaminifu.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (01/581)
  • Imechapishwa: 04/06/2018
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy