12. Fadhilah ya nne ya funga: Harufu ya mfungaji inapendwa zaidi na Allaah


4- Harufu ya mfungaji ni nzuri zaidi mbele ya Allaah kuliko harufu ya miski kwa sababu imetokana na athari ya funga. Kwa hiyo ndio maana ikawa ni nzuri zaidi mbele Yake (Subhaanah) na yenye kupendwa Kwake. Hii ni dalili juu ya utukufu wa jambo la swawm mbele ya Allaah kiasi cha kwamba kitu chenye kuchukizwa na kibaya mbele ya watu kinakuwa ni chenye kupendwa na kizuri mbele ya Allaah kwa sababu kimetokana na kumtii kwa kufunga.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 16
  • Imechapishwa: 08/04/2020