12. Du´aa ya kwenda msikitini


اللَّهُمَّ اجْعَلْ فِي قَلْبِي نُوراً، وَفِي لِسَانِي نُوراً، وَفِي سَمْعِي نُوراً، وَفِي بَصَرِي نُوراً، ومِنْ فَوْقِي نُوراً، وَمِنْ تَحْتِي نُوراً، وَعَنْ يَمِينِي نُوراً، وَعَنْ شِمَالِي نُوراً، وَمِنْ أمَامِي نُوراً، وَمِنْ خَلْفِي نُوراً، واجْعَلْ في نَفْسِي نُوراً، وأعْظِمْ لِي نُوراً، وَعَظِّمْ لِي نُوراً، واجْعَلْ لِي نُوراً، وَاجْعَلْنِي نُوراً، اللَّهُمَّ أعْطِنِي نُوراً، واجْعَلْ فِي عَصَبِي نُوراً، وَفِي لَحْمِي نُوراً، وَفِي دَمِي نُوراً، وفِي شَعْرِي نُوراً، وفِي بَشَرِي نُوراً

اللَّهُمَّ اجْعَلْ لِي نُوراً فِي قَبْرِي … ونُوراً فِي عِظَامِي

وَزِدْنِي نُوراً، وَزِدْنِي نُوراً، وَزِدْنِي نُوراً

وَهَبْ لِي نُوراً عَلَى نُورٍ

“Ee Allaah! Weka ndani ya moyo wangu nuru, katika ulimi wangu nuru, usikizi wangu nuru, uoni wangu nuru, juu yangu nuru, chini yangu nuru, kuliani kwangu nuru, kushotoni kwangu nuru, mbeleni kwangu nuru, nyumani kwangu nuru, weka ndani ya moyo wangu nuru, nifanyie kubwa nuru yangu, nyingi nuru yangu, niwekee mimi nuru, nifanyie mimi nuru. Ee Allaah! Nipe nuru, uweke katika mishipa yangu nuru, katika nyama zangu nuru, katika damu yangu nuru, katika nywele zangu nuru na katika ngozi yangu nuru.”[1]

“Ee Allaah! Niwekee mimi nuru ndani ya kaburi langu… na nuru katika mifupa yangu.”[2]

“Unizidishie nuru, Unizidishie nuru na Unizidishie nuru.”[3]

“Na unipe Unitunuku nuru ya nuru.”[4]

[1] Tazama mkusanyiko wa matamshi yote haya katika “al-Bukhaariy” (6316) na Muslim (529) na (529) na (530) na (763).

[2] at-Tirmidhiy (3419).

[3] al-Bukhaariy katika “Aadab-ul-Mufrad” (695) uk. 258. Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh al-Aadab al-Mufrad” (536).

[4] Tazama “al-Fath” (11/118).

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 15/07/2018