[16] Ni Sunnah kusema mwishoni mwa Witr, ni mamoja iwe kabla au baada ya Tasliym:

اللهم إني أعوذ برضاك من سخطك, وبمعافاتك من عقوبتك، وأعوذ بك منك، لا أحصي ثناءً عليك, أنت كما أثنيت على نفسك

“Ee Allaah! Hakika mimi najilinda kwa ridhaa Yako kutokamana na hasira Zako, msamaha Wako kutokamana na adhabu Yako na naomba ulinzi Kwako kutokamana na Wewe. Siwezi kukusifu vile Unavostahiki Wewe ni kama vile Ulivyojisifu Mwenyewe.”[1]

[18] Baada ya kumaliza Witr, mtu aseme:

سبحان الملك القدوس, سبحان الملك القدوس, سبحان الملك القدوس

“Ametakasika Mfalme, Mtakatifu. Ametakasika Mfalme, Mtakatifu. Ametakasika Mfalme, Mtakatifu.”

Sauti inatakiwa kurefushwa na kuiinua mara ya tatu[2].

[1] Swahiyh Abiy Daawuud (1282) na “al-Irwaa´” (430).

[2] Swahiyh Abiy Daawuud (1284).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qiyaam Ramadhwaan, uk. 32-33
  • Imechapishwa: 07/05/2019