12. Dalili juu ya mguu wa Allaah 12

12- Ja´far bin Muhammad bin Ya´quub as-Sandaliy ametuhadithia: al-Hasan bin Muhammad az-Za´faraaniy ametuhadithia: Shabaabah ametuhadithia: Warqaa´ ametuhadithia, kutoka kwa Abuz-Zinaad, kutoka kwa al-A´raj, kutoka kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:

“Pepo na Moto vilizozana ambapo Moto ukasema: “Ndani yangu wanaingia wakandamizaji na wenye kiburi.” Pepo nayo ikasema: “Ndani yangu wanaingia watu wadhaifu na wale masikini.” Ndipo Allaah (´Azza wa Jall) akasema kuiambia Pepo: “Wewe ni huruma Yangu ambayo namsibu yule Ninayemtaka katika waja Wangu.” Akasema kuuambia Moto: “Wewe ni adhabu Yangu ambayo namsibu yule Ninayemtaka katika waja Wangu. Kila mmoja wenu atajazwa.” Kuhusu Moto hautojaa mpaka pale Atapoweka unyayo Wake juu yake mpaka useme: “Tosha, tosha.” Hapo ndipo utajaa na ujikusanye.”

Hivyo ndivyo alivyopokea Muslim bin al-Hajjaaj, kupitia kwa Muhammad, kutoka kwa Naafiy´, kutoka kwa Shabaabah, kutoka kwa Warqaa´.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 46-47
  • Imechapishwa: 05/11/2017