12. Alipe Dhuhr na ´Aswr pamoja na Maghrib na ´Ishaa?

Swali 12: Akitwahirika mwenye hedhi au mwenye damu ya uzazi wakati wa ´Aswr analazimika kulipa Dhuhr pamoja na ´Aswr au inayomlazimu ni ´Aswr peke yake?

Jibu: Maoni yenye nguvu katika masuala haya ni kwamba analazimika kulipa ´Aswr peke yake. Kwa sababu hakuna dalili juu ya ulazima wa kulipa Dhuhr. Msingi ni kutakasika kwa dhimmah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kuwahi Rak´ah moja ya swalah ya asubuhi kabla ya jua kuchomoza basi ameiwahi ´Aswr.”

Hakutaja kwamba ameiwahi Dhuhr. Dhuhr ingelikuwa ni lazima basi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) angebainisha.

Jingine ni kwmaba mwanamke akipata hedhi baada ya kuingia wakati wa Dhuhr hakuna kinachomlazimu isipokuwa kulipa swalah ya Dhuhr pasi na swalah ya ´Aswr ingawa wakati fulani Dhuhr inakusanywa pamoja na ´Aswr. Hapana tofauti kati yake na sura ya swali lililoulizwa.

Kujengea juu ya haya ni kwamba maoni yenye nguvu ni kwamba hakuna kinachomlazimu isipokuwa kulipa ´Aswr peke yake kwa dalili ya andiko na kipimo.

Vivyo hivyo ndio hali endapo mwanamke atasafika kabla ya kumalizika kwa wakati wa ´Ishaa. Katika hali hiyo hakuna kinachomlazimu isipokuwa swalah ya ´Ishaa peke yake. Swalah ya Maghrib haimlazimu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 13-14
  • Imechapishwa: 20/06/2021