Baada ya mtunzi (Rahimahu Allaah) kumswalia na kumtakia amani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ndipo akakiswalia na kukitakia amani kizazi chake. Kizazi cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni wale waumini katika jamaa zake ambao haifai kwa wao kuchukua zakaah: familia ya al-´Abbaas, familia ya ´Aliy, familia ya ´Aqiyl na familia ya Ja´far. Hawa ndio jamaa na kizazi cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Vilevile katika kizazi chake wanaingia wale wafuasi wa dini yake. Kila ambaye anamfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumwamini anaingia katika kizazi chake lakini hata hivyo sio katika jamaa zake. Kizazi kimegawanyika sampuli mbili: wale ambao ni jamaa na wale ambao ni wafuasi wa dini. Ujamaa umekusanya kati ya fadhilah mbili: udugu na imani. Maswahabah zake pia wanaingia ndani ya kizazi chake inapokuja katika ufuasi, lakini mtunzi amewataja kipekee kwa ajili ya kutilia mkazo haki yao. Isitoshe wao ndio walikuwa Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao walimwamini, wakamtukuza, wakamnusuru na wakapambana bega kwa bega pamoja naye. Wao wako na fadhilah juu ya Ummah huu. Hakuna mwengine hata mmoja anayeweza kufikia fadhilah za Maswahabah, pasi na kujali imani na kumcha Allaah kiasi gani watakuwa nako wale waliokuja nyuma yao. Muda wa kuwa walikuwa ni Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi wao ndio watu bora wa Ummah huu. Hakuna yeyote anayeshirikiana nao katika hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 91-92
  • Imechapishwa: 08/09/2021