118. Du´aa ya kusimama kati ya Swafaa na Marwah

  Download236- Wakati (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokurubia Swafaa alisoma:

إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَآئِرِ اللّهِ

“Hakika vilima vya Swafaa na Marwah ni katika alama za Allaah.”[1]

Naanza kwa kile alichoanza kwacho Allaah.”

Akaanza kwa Swafaa, akapanda mpaka akaiona Ka´bah, akaelekea Qiblah ambapo akampwekesha Allaah na kusema:

الله أكبر لا إله إلا الله وحده لا شريك له له الملك وله الحمد يحيي ويميت وهو على كل شيء قدير

لا إله إلا الله وحده لا شريك له أنجز وعده ونصر عبده وهزم الأحزاب وحده

“Allaah ni mkubwa. Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa peke yake hana mshirika. Ufalme ni Wake Yeye na himdi zote ni Zake Yeye. Anahuisha na Anafisha. Naye juu ya kila jambo ni muweza. Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa peke yake hana mshirika. Ameitimiza ahadi Yake, amemnusuru mja Wake na amevishinda vikosi hali ya kuwa peke yake.”

Kisha akaomba du´aa baina yake. Alisema mfano wa maneno hayo mara tatu… “

Ndani yake imekuja:

“Akafanya katika Marwah kama alivofanya katika Swafaa.”[2]

[1] 02:158

[2] 02:258 Muslim (02/888).

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: www.firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 08/05/2020