118. al-Qummiy upotoshaji wake wa kwanza wa al-An´aam


al-Qummiy amesema pindi alipokuwa akifasiri Aayah:

وَلَوْ تَرَىٰ إِذْ وُقِفُوا عَلَى النَّارِ فَقَالُوا يَا لَيْتَنَا نُرَدُّ وَلَا نُكَذِّبَ بِآيَاتِ رَبِّنَا وَنَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ

“Lau ungeliona watakaposimamishwa katika moto halafu wakasema: “Laiti tungelirudishwa na wala hatutakadhibisha Aayah za Mola wetu na tutakuwa miongoni mwa waumini.”[1]

“Imeteremshwa kuhusu Banuu Umayyah. Kisha akasema:

بَلْ بَدَا لَهُم مَّا كَانُوا يُخْفُونَ مِن قَبْلُ

“Bali yamewadhihirikia yale waliyokuwa wakiyaficha hapo kabla… ”[2]

Bi maana uadui/chuki zao kwa kiongozi wa waumini.

وَلَوْ رُدُّوا لَعَادُوا لِمَا نُهُوا عَنْهُ وَإِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ

“… na lau wangelirudishwa, basi hakika wangeyarudia yale waliyokatazwa na hakika wao ni waongo.” [3][4]

Katika Aayah hizi mbili Allaah anataja hali za makafiri ambao wamewakufuru Mitume na yale waliyokuja nayo katika Tawhiyd na kukataza kwao kumshirikisha Allaah. Wamekadhibisha Vitabu na yale yaliyomo ndani yake katika kufufuliwa, malipo, hesabu, Pepo na Moto. Pindi watapoona neema za Peponi na hali zengine zote, minyororo na pingu watasema hali ya kuhuzunika na kusikitika:

يَا لَيْتَنَا نُرَدُّ وَلَا نُكَذِّبَ بِآيَاتِ رَبِّنَا وَنَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ

“Laiti tungelirudishwa na wala hatutakadhibisha Aayah za Mola wetu na tutakuwa miongoni mwa waumini.”

Bi maana yale yote waliyokuja nayo Mitume.

Halafu Baatwiniy huyu anazijia Aayah hizi tukufu zinazohusu maana hii kubwa na yale yanayowasubiri makafiri na maadui wa makafiri na kuzipindisha katika yale yaliyozuliwa na Baatwiniyyah Faafidhwah kuhusu Banuu Umayyah na uadui wao kwa kiongozi wa waumini. Kwa msemo mwingine ni kwamba Aayah zinapindishwa kwenda katika I´tiqaad zao za batili. Sambamba na hilo  makafiri wote na maadui wa Mitume ambao waliwakadhibisha, wakawafanyia inadi, wakawatuhumu uchawi, uongo na wakaita yale waliyokuja nayo kwamba ni pumba wanasitiriwa. Matishio haya makali yanayowaelekea makafiri waliowakadhibisha Mitume yanafichwa. Kitendo chao hichi kinamkadhibisha Allaah na Qur-aan na kinayabomoa makusudio na zile faida nyingi ambazo hakuna anayezitambua isipokuwa yule ambaye anamuadhimisha Allaah, Qur-aan na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ukweli wa kumuadhimisha.

[1] 06:27

[2] 06:28

[3] 06:28

[4] Tafsiyr al-Qummiy (1/196).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 175-176
  • Imechapishwa: 02/06/2018