Swali 117: Ni ipi hukumu ya kuyatembelea makaburi kufanya maalum siku ya ijumaa?

Jibu: Ni jambo lisilokuwa na msingi. Lililowekwa katika Shari´ah ni yule mwenye kuyatembelea makaburi ayatembelee wakati wowote itapokuwa sahali. Ni mamoja ikawa usiku au mchana. Kuhusu kuyatembelea siku maalum au usiku maalum ni Bid´ah isiyokuwa na msingi wowote. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yeyote atakayezua katika amri yetu hii yale yasiyokuwemo basi atarudishiwa mwenyewe.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

“Yeyote atakayefanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu basi atarudishiwa mwenyewe.”[2]

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa).

[1] al-Bukhaariy (2697) na Muslim (1718).

[2] Muslim (1718).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 87
  • Imechapishwa: 13/01/2022