116. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa nne wa al-Maa-idah

al-´Ayyaashiy amesema:

“Yaziyd al-Kinaasiy amesema: “Nilimuuliza Abu Ja´far kuhusiana na Aayah:

يَوْمَ يَجْمَعُ اللَّـهُ الرُّسُلَ فَيَقُولُ مَاذَا أُجِبْتُمْ ۖ قَالُوا لَا عِلْمَ لَنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ

“Siku Allaah atawakusanya Mitume na kuwaambia: “Mlijibiwa nini?” Watasema: “Hatuna ujuzi nalo, kwani hakika Wewe unayajua mno yenye kufichikana.”[1]

Akasema: “Mlijibu nini juu ya wasii wenu ambao mmewaacha nyuma kwa nyumati zenu?” Watasema: “Hatujui ni nini wamefanya baada yetu.”[2]

Mhakiki amerejesha kwa “al-Burhaan” na “al-Bihaar”.

Allaah amemtakasa Abu Ja´far kutokamana na uongo huu juu ya Qur-aan.  Maana ya Aayah ni kwamba Allaah atawakusanya Mitume wote siku ya Qiyaamah ili kuwauliza juu ya kuitikia kwa nyumati zao juu ya ulinganizi wao kwa Allaah, Tawhiyd na Shari´ah nyenginezo na kuhusu kuitikia kwao juu ya kufufuliwa, hesabu na malipo. Kule Allaah kuwauliza Mitume Wake mbele ya nyumati zao katika Siku hiyo yenye kutisha kuna makemeo kwa wale wote waliowakadhibisha na kuwakufuru na kukufuru yale waliokuja nayo. Allaah atawauliza Mitume na aziulize nyumati. Amesema (Ta´ala):

فَلَنَسْأَلَنَّ الَّذِينَ أُرْسِلَ إِلَيْهِمْ وَلَنَسْأَلَنَّ الْمُرْسَلِينَ

“Basi bila ya shaka Tutawauliza wale ambao waliopelekew ujumbe na bila shaka Tutawauliza Mitume.”[3]

يَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ مَاذَا أَجَبْتُمُ الْمُرْسَلِينَ فَعَمِيَتْ عَلَيْهِمُ الْأَنبَاءُ يَوْمَئِذٍ فَهُمْ لَا يَتَسَاءَلُونَ

”Siku Atakapowaita aseme: “Mliwajibu nini Mitume?” Basi Siku hiyo zitawafichikia khabari nao hawatoweza kuulizana.”[4]

Allaah hatowauliza Mitume Wake jengine isipokuwa tu kuhusu wasii wao? Hilo si jengine isipokuwa ni fikira za kiyahudi zilizozuliwa na Ibn Sabaa´ myahudi. Raafidhwah Baatwiniyyah wamesimama na kazi ya kukikengeusha Kitabu cha Allaah kwa sababu yake na yale yote yenye kuhusiana nao katika batili.

[1] 05:109

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/349).

[3] 07:06

[4] 28:65-66

  • Mhusika: Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 172-173
  • Imechapishwa: 10/05/2018