114. al-Qummiy upotoshaji wake wa nne wa al-Maa-idah


al-Qummiy amesema wakati alipokuwa akifasiri Aayah:

قَدْ جَاءَكُم مِّنَ اللَّـهِ نُورٌ وَكِتَابٌ مُّبِينٌ

“Hakika imekufikieni kutoka kwa Allaah nuru na Kitabu kinachobainisha.”[1]

“Nuru ni kiongozi wa waumini na maimamu.”

Huu ni uongo na ujasiri juu ya kukipotosha Kitabu cha Allaah. Nuru ni Uislamu na Kitabu kinachobainisha ni Qur-aan.

[1] 05:15

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 161-162
  • Imechapishwa: 24/04/2018