Umesikia. Allaah akurehemu. Unasubiriwa na njia hii yenye matatizo, njia nzito, daraja yenye kutisha na kizingiti kigumu ambacho miguu haiwezi kuwa imara kwayo wala mawazo hayawezi kuyafikiria. Hakuna atayekuwa imara isiipokuwa yule atayefanywa kuwa thabiti na Allaah kwa maneno. Huenda mghafilikaji aliyekosa uwafikishwaji ataposikia kunazungumziwa Njia atadhani kuwa ni kama uzito unaopatikana katika njia za hapa duniani zisizokuwa na kupanda na kushuka. Mbali kabisa. Hajui. Ninaapa kwa Allaah kuwa ina makali zaidi kuliko upanga na ni nyembamba zaidi kuliko unywele. Upande wake wa kulia kuna ndoano na miba.

Njia itakuwa katika hali hii pindi utakuwa huna budi ya kupita juu yake. Baya kuliko yote ni kuwa Moto uko chini yako. Moyo wako utashtuka pindi utapoona hali hii. Masikio yako yatajaa mgurumo wake. Je, utaweza kupita, kusimama au kutambaa? Utapopatwa na uzito wakati wa kupita na moto chini umeshika kwelikweli hakuna kingine kitachokunufaisha isipokuwa matendo mema au tawbah ya kweli kutokamana na madhambi. Chagua hivi sasa ni matendo gani yatayokufanya ufaulu na ni njia ipi itayokunufaisha. Ibn Abiy Dunyaa amepokea kwa mlolongo wa wapokezi wake kwamba Wahb bin Munabbih amesema:

“Nilisoma kwenye Zabuur ya Daawuud: “Allaah (Ta´ala) alisema: “Ee Daawuud! Unajua ni kina nani wataopita kwa haraka juu ya Njia? Ni wale wenye kuridhia hukumu Yangu na ndimi zao zinapatwa na unyevunyevu kwa sababu ya kunitaja.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 233
  • Imechapishwa: 24/12/2016