113. Jawabu juu ya Hadiyth “Mche Allaah na subiri”

Swali 113: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema:

“Mche Allaah na subiri.”[1]

kumwambia mwanamke ambaye alimwona analia karibu na kaburi kuna dalili inayoonyesha kuwa inafaa kwa mwanamke kuyatembelea makaburi[2]?

Jibu: Pengine haya yalitokea kipindi ambapo yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa amewapa idhini wote wanamme na wanawake kuyatembelea. Kwa sababu Hadiyth zinazowakataza wanawake kuyatemebela makaburi ni zenye kuhukumu na zinafuta zote zilizoko kabla yake.

[1] Ahmad (12049), al-Bukhaariy (1252) na Muslim (926).

[2] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/331-332).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 85
  • Imechapishwa: 09/01/2022