113. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa pili wa al-Maa-idah


al-´Ayyaashiy amesema:

“Zaraarah amepokea kutoka kwa Abu Ja´far ambaye amesema: “Faradhi ya mwisho iliyoteremshwa ni uongozi:

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا

“Leo Nimekukamilishieni dini yenu na nimekutimizieni neema Yangu na nimekuridhieni kwenu Uislamu iwe dini yenu.”[1]

Baada ya hapo hakuna faradhi zengine zilizoteremshwa mpaka Allaah akamchukua Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[2]

Tazama namna ambavyo Raafidhwiy na Baatwiniy huyu anavyoyakengeusha maneno ya Allaah na kupindisha maana ya Allaah tukufu kwa njia waliyozuliwa na Ibn Sabaa´! Yeye na wafuasi wake wamepotosha sehemu kubwa ya Qur-aan kwa sababu ya jambo hili lililozuliwa la uongozi na wasia. Amesema:

“Ja´far bin Muhammad al-Khuzaa´iy amepokea kutoka kwa baba yake ambaye amesimulia ya kwamba amemsikia Abu ´Abdillaah akisema: Wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipotua ´Arafah siku ya ijumaa alijiwa na Jibriyl (´alayhis-Salaam) na akamwambia: “Ee Muhammad! Hakika Allaah anakutolea salamu na anakwambia uwaambie Ummah wako:

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا

“Leo Nimekukamilishieni dini yenu na nimekutimizieni neema Yangu na nimekuridhieni kwenu Uislamu iwe dini yenu.”[3]

Baada ya haya sintokuteremshia kitu kingine. Tayari nimeshakuteremshia swalah, zakaah, swawm na hajj. Hili ni la tano. Sintoyakubali haya mane isipokuwa pamoja na hili.”

Tayari maneno yangu yameshakariri juu ya uzushi wao wa uongozi huu ambao kwa ajili yake wanaipotosha Qur-aan. Jipya hapa ni kwamba ameziangusha Shari´ah za imani zote isipokuwa mambo haya mane na akafanya uongozi ndio badala yake. Moja katika Shari´ah hizi ni kushuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah na nguzo za imani ni kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, siku ya Mwisho na Qadar kheri na shari yake, kupambana katika njia ya Allaah na Shari´ah nyenginezo. Ni kumzulia Allaah uongo kwa sampuli gani na kucheza na dini Yake unaweza kupimwa uzushi na mchezo huu?

[1] 05:03

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/292).

[3] 05:03

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 161
  • Imechapishwa: 23/04/2018