Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

السلام علينا و على عباد الله الصالحين

“Amani ishuke juu yetu na juu ya waja wema wa Allaah.”

Wajiombea salaam mwenyewe na kwa kila kiumbe mwema katika mbingu na ardhi. as-Salaam ni du ´aa huombewa waja wema lakini haitakiwi kuwaomba wao pamoja na Allaah.

MAELEZO

Maneno yake:

“… katika mbingu… “

Nao ni Malaika.

Maneno yake:

“… na ardhi.”

Ambao ni waumini katika watu na majini. Kila kiumbe mwema mbinguni na ardhini inamkusanya du´a hii.

Maneno yake:

“as-Salaam ni du ´aa huombewa waja wema lakini haitakiwi kuwaomba wao pamoja na Allaah.”

Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) anawaraddi wale wanaowaabudia wafu waliyomo ndani ya makaburi kwa madai ya kwamba eti ni waja wema na hivyo wanawaomba badala ya Allaah. Bali wanaombewa du´aa. Wao ni wenye kukuhitajia uwaombee msamaha na rehema. Watu hawa ni wenye kupewa mtihani ndani ya makaburi yao na hawamiliki juu ya nafsi zao – sembuse juu ya nafsi za wengine – manufaa na wala hawawezi kujiondoshea yale waliyomo. Vipi basi utawaomba wao badala ya Allaah? Vipi unawaomba wakufanyie uombezi, wakutajirishe na wakuondoshee matatizo ilihali mwili wake umekwishaoza na ni mwenye kukuhitajia wewe? Ziko wapi akili za washirikina?

Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) amenyofoa hukumu kutoka katika Tashahhud maana ya kumtakasia ´ibaadah Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com