Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Kwamba mimi namkufurisha Ibn-ul-Faaridhw na Ibn ´Arabiy na kwamba mimi nimetia moto “Dalaa-il-ul-Khayraat” na “Rawdh-ur-Rayaahiyn” na kwamba nakiita “Rawdh-ush-Shayaatwiyn”[1].

MAELEZO

Ibn-ul-Faaridhw ni yule mtunzi wa utenzi wa “at-Taa-iyyah” kuhusu Wahdat-ul-Wujuud. Ndani yake mna ukafiri. Lakini hata hivyo Shaykh hamkufurishi mtunzi wacho. Kwa sababu Shaykh hajui alikufa akiwa na hali gani. Jengine hajui kama alifikiwa na hoja au hakufikiwa. Msimamo wake ni kwamba anaona kuwa yaliyomo ndani yake ni ukafiri na shirki. Lakini mtunzi wacho anachukua msimamo wa kunyamaza. Haya ndio madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Wao hawashuhudii Pepo wala Moto juu ya yeyote isipokuwa tu yule aliyeshuhudiwa na Mtume wa Allaah  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Ibn ´Arabiy anatambulika. Ni Muhy-id-Diyn bin ´Arabiy at-Twaa-iy ambaye ndiye kiongozi wa Wahdat-ul-Wujuud. Ibn-ul-Faaridhw ni mmoja katika wafuasi wa Ibn ´Arabiy. Pamoja na haya Shaykh hakati moja kwa moja juu ya ukafiri wao. Ijapokuwa alisema ukafiri, upotevu na ukanamungu. Lakini kumkufurisha mtu kwa dhati yake ni jambo linahitajia dalili. Kwa sababu pengine alitubia. Pengine hali yake ya mwisho alikhitimisha kwa tawbah. Allaah ndiye anajua zaidi.

Miongoni mwa uongo dhidi ya Shaykh ni pale wanaposema kuwa alitia moto “Dalaa-il-ul-Khayraat”. Kitabu hicho kinazungumzia “as-Swalaatu was-Salaam ´alaa Khayr-il-Bariyyaat”. Ndani yake mna uchupaji mpaka. Ndani yake anaombwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni kitabu ambacho ndani yake mna batili. Lakini Shaykh hakichomi moto. Lakini alikuwa akiusia kusoma vitabu vyenye faida ambavyo havina upindaji.

Vivyo hivyo “Rawdh-ur-Rayaahiyn”. Pia ni kitabu kinachovuka mpaka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini Shaykh kukichoma moto hakupelekei katika natija.

Wakamzulia Shaykh na wakasema kwamba amekiita “Rawdh-ush-Shayaatwiyn”. Yote haya ni kumsemea uongo Shaykh (Rahimahu Allaah).

[1] Tazama ”Swiyaanatu al-Insaan ´alaa waswasat-is-Shaykh Dahlaan”, uk. 504-505.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 155
  • Imechapishwa: 09/06/2021