Maradhi yanayomfanya kushindwa kusoma al-Faatihah

Swali: Mimi ni kijana ambaye yamenipata maradhi ya neva na nimefikwa na siku ambazo nashindwa kutamka al-Faatihah. Kuna ndugu nimemtuma kwa mmoja katika Mashaykh akanijibu kwamba inafaa kwangu kuswali kwa kiwango cha Rak´ah pasi na kisomo. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Mola wetu amesema:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.” (64:16)

Muislamu akipatwa na jambo linalomfanya kushindwa kusoma, swalah yake inasihi. Atasimama kwa kiwango cha kusoma al-Faatihah na kilicho zaidi yake kidogo na kunamtosha. Akiweza kusema Subhaan Allaah, Alhamdulillaah, Laa ilaaha illa Allaah na Allaahu Akbar, basi itamuwajibikia kufanya hivo. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha kufanya Tasbiyh, Tahmiyd, Tahliyl, Takbiyr na Laa hawlah wa quwattah illa bi Allaah yule ambaye alimlalamikia kushindwa kusoma al-Faatihah. Pia anaweza kusema yale yatayomkuwia wepesi katika mfano wa hayo. Anayeweza kufanya hivo basi atafanya mpaka pale atakapoweza kusoma al-Faatihah. Tunacholenga ni kwamba:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4317/ما-حكم-صلاة-العاجز-عن-القراءة
  • Imechapishwa: 06/06/2022