111. Ni ipi hukumu mwanamke kuyatembelea makaburi?


Swali 111: Ni ipi hukumu mwanamke kuyatembelea makaburi[1]?

Jibu: Haijuzu kwa wanawake kuyatembelea makaburi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani wanawake wenye kuyatembelea makaburi. Jengine wanawake ni fitina na subira yao ni chache. Miongoni mwa rehema na wema wa Allaah ndipo akawaharamishia kuyatembelea makaburi ili wasije kufitinisha wengine au wao wakafitinishwa.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/325).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 84
  • Imechapishwa: 12/01/2022