Ibn-ul-Jawziy ametaja katika “ath-Thabaat ´alaal-Mawt” kupitia kwa ´Aliy bin al-Muwaffaq aliyesimulia kuwa alimsikia Haatim al-Asamm akisema:

“Tulianza kupigana na waturuki. Mturuki mmoja akanipiga mshale na nikaanguka juu ya farasi wangu. Akateremka kwenye farasi wake, akakaa juu ya kifua changu na akanishika taya zangu. Akatoa nje kisu chake ili anichinje. Ninaapa kwa Mola wangu sikuwa namfikiria si yeye wala kisu chake – nilichokuwa nafikiria ni Mola wangu ni kipi alichonipangia na nikajiambia mwenyewe: “Mola wangu! Ikiwa umenipangia anichinje basi niko radhi. Mimi ni Wako na ni mali Yako.” Wakati nilipokuwa nafikiria hivo huku yeye amenikalia juu ya kifua. Tahamaki muislamu mmoja akampiga mshale shingoni na akaanguka kutoka kwangu. Nikamsimamia, nikachukua kisu kutoka mkononi mwake na nikamchinja nacho. Si vyengine isipokuwa inahusiana na mioyo yenu iwe kwa Mfalme wenu. Hapo ndipo mtaona Alivyo na upole zaidi kwenu kuliko wazazi wenu.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 230-231
  • Imechapishwa: 22/12/2016