110. Mwisho wa “Swifatu Swalaat-in-Nabiy”

Yote yaliyotangulia juu ya sifa ya swalah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhiwa sallam) yanawahusu wanaume kama ambavo vilevile yanawahusu wanawake. Hakukuthibiti dalili katika Sunnah kinachoonyesha kuwa swalah ya mwanamke inaswaliwa kinyume. Bali ueneaji wa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhiwa sallam):

“Swalini kama mlivyoniona nikiswali.”

yanawakusanya wanaume na wanawake pia. Ibraahiym an-Nakha´iy amesema:

“Mwanaume anatakiwa kuswali kama anavoswali mwanaume.”[1]

Hadiyth inayosema kuwa mwanamke ajikusanye katika Sujuud na kwamba asifanye kama anavofanya mwanaume kuna Swahabah anayekosekana katika cheni ya wapokezi na haisimamishi hoja yoyote. Ameipokea Abu Daawuud katika “al-Maraasiyl”[2] kupitia kwa Yaziyd bin Abiy Habiyb. Imetajwa katika “adh-Dhwa´iyfah”[3].

Kuhusu yale aliyopokea Imaam Ahmad ya kwamba Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) aliwaamrisha wanawake zake waswali hali ya kukaa mkao wa kimarufaa, haikusihi cheni ya wapokezi wake. Kwa sababu ndani yake yumo ´Abdullaah bin ´Umar al-´Umariy ambaye ni dhaifu[4].

al-Bukhaariy amepokea katika ”at-Taariykh as-Swaghiyr”[5] kwa mlolongo wa wapokezi ulio Swahiyh ya kwamba Umm-ud-Dardaa´ (ambaye alikuwa mwanamke msomi) alikuwa akikaa katika swalah kama akaavyo mwanaume.

Mpaka hapa ndipo mwisho wa kitabu kuhusu swalah ya Mtume wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhiwa sallam) kuanzia katika Takbiyr mpaka katika Tasliym. Namuomba Allaah (Ta´ala) ajaalie niwe nimeifanya kwa imani kabisa kwa ajili ya kutafuta uso Wake mtukufu na kiongoze katika Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhiwa sallam) mpole na mwenye kurehemu.

سُبْحانَكَ اللهُمَّ وَبِحَمْدِكَ أَشْهَدُ أَنْ لا إِله إِلا أَنْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتُوبُ إِلَيْكَ

Kutakasika kutokamana na mapungufu na himdi zote ni Zako, ee Allaah. Nashuhudia ya kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Wewe. Nakuomba msamaha na nakutubia Kwako.

اللهم صل على محمد و على آل محمد و بارك على محمد و على آل محمد كما صليت و باركت على إبراهيم و آل إبراهيم، إنك حميد مجيد

“Ee Allaah! Msifu Muhammad na jamaa zake Muhammad na mbariki Muhammad na jamaa zake Muhammad kama Ulivyomsifu na kumbariki Ibraahiym na jamaa zake Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa.

[1] Ibn Abiy Shaybah (2/75/1) kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

[2] 87/117.

[3] 2652.

[4] Masaa-il-ul-Imaam Ahmad, uk. 71, ya mtoto wake ´Abdullaah.

[5] Uk. 95

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 165
  • Imechapishwa: 15/01/2019