11. Zima Taa!


Siku moja nilikaa kwenye darsa ya Hasan al-Bannaa. Alikuwa akifafanua Hadiyth ya yule mtu mwenye kuswali vibaya. Ilipofika wakati wa swalah Shaykh mmoja kutoka Azhar akiitwa Shaykh Jawhar akatangulia mbele kuongoza swalah. Akatuswalisha mbio mbio kama jogoo mwenye kudokoa. Nikamwambia Hasan al-Bannaa: “Ee Shaykh! Inaonekana kama kwamba ambaye ametuongoza katika swalah amefahamu kuwa yule mtu aliyeswali vibaya aliswali vizuri.” Nikamuomba amnasihi. Pamoja na hivyo hakumnasihi na akajaribu kubadilisha maudhui. Ndipo nilipojua kuwa al-Ikhwaan al-Muslimuun wanacholenga sio kuzitengeneza hali za watu.

Baada ya hapo nikakutana na baadhi ya marafiki ikiwa ni pamoja na Hasan Jamaaliy na Muhammad Bashshaar. Hasan Jamaaliy alikuwa ni mtu mwenye kuitetea ´Aqiydah sahihi. Nikawaambia: “Mtu huyu amepinda.” Wakanambia: “Vipi itakuweje ilihali anamtaja Ibn Taymiyyah na Ibn-ul-Qayyim?” Baada ya muda akaja Muhammad Bashshaar na kunambia: “Uliyosema ni kweli.” Nikamwambia: “Kumepitika nini?” Akanambia: “Jana kulikuwa kikao na Shaykh kutoka kwenye pote la Suufiyyah nyumbani kwa Hasan al-Bannaa. Hasan al-Bannaa akauliza: “Hasan Jamaaliy yuko hapa?” Wakasema: “Hapana.” Akauliza tena: “Mahmuud yuko hapa?” Wakasema: “Hapana.” Ndipo Hasan al-Bannaa akasema: “Basi tuzime taa sasa na kumkumbuka Allaah.”

Hasan al-Bannaa anajaribu makundi na madhehebu yote kufanya yawe na umoja. Anazungumza na watu vile madhehebu yao yalivo. Akizungumza na Shaafi´iy hutamka maoni ya ash-Shaafi´iy. Mkutano wangu wa mwisho na Hasan al-Bannaa ilikuwa mwaka wa 1937.

Mwandishi: Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Bannaa
Marejeo: Lamahaat ´an Da´wat-il-Ikhwaan al-Muslimiyn, uk. 33-34
Mkusanyaji: Muhammad bin ´Iwadhw bin ´Abdil-Ghaniy