Swali 11: Kwa mfano Jamaa´at-ut-Tabliygh wanasema kuwa wanataka kufuata mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na inaweza kutokea baadhi yao wakakosea. Hivyo wanauliza ni vipi mnaweza kuwahukumu na kutahadharisha juu yetu?

Jibu: Watu waliotoka na kuwasoma Jamaa´at-ut-Tabliygh wameandika juu yao. Wameandika mengi kuhusu wao na makosa kwa undani waliyotumbukia ndani. Hivyo basi someni vitabu vilivyoandikwa juu yao ili muweze kubainikiwa na suala hili[1].

[1] Miongoni mwa watu walioandika kuhusu Jamaa´at-ut-Tabliygh na kufanya vizuri, kunufaisha na kuweka wazi fikira zao ni muheshimiwa Shaykh Sa´d bin ´Abdir-Rahmaan al-Huswayyin katika kitabu “Haqiyqat-ud-Da´wah ilaa Allaah (Ta´ala)” kilichotolewa chini ya uoni wa Shaykh Faalih bin Naafiy´ al-Harbiy. Amesema wakati alipoingia kwenye maana ya ´Laa ilaaha illa Allaah` kwa mujibu wa Jamaa´at-ut-Tabliygh:

“Maana yake ni kuondosha yakini ya vitu vilivyoharibika kutoka moyoni na badala yake kuingiza yakini sahihi kuhusu dhati ya Allaah na kwamba hakuna muumbaji yeyote isipokuwa Allaah, hakuna mwenye kuruzuku yeyote isipokuwa Allaah na hakuna mwenye kuyaendesha mambo isipokuwa Allaah.”

Hili kwa hakika hakuna jengine zaidi ya Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah ambayo ilikuwa inakubaliwa na washirikina wa zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Pamoja na hivyo halikuwaingiza ndani ya Uislamu.” (Uk. 70)

Amesema pia:

“Fikira zao ni kwamba wao ni Ahnaaf katika Fiqh, Ash´ariyyah na Maaturiydiyyah katika ´Aqiydah na Jishtiyyah, Naqshbandiyyah, Qaadiriyyah na Sahrawardiyyah katika Taswawwuf.” (Uk. 80)

Vilevile Shaykh Hamuud bin ´Abdillaah at-Tuwayjiriy (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu cha kipekee kuhusu wao. Kitabu chake kimeingia kwa undani zaidi kuhusu pote hili. Kitabu kimeweka wazi uhakika wao uliotolewa kutoka katika vitabu vyao. Makosa yao yameraddiwa humo. Ukiongezea juu ya hilo ni kwamba amenukuu mashahidi wa kuaminika ambao wana uzowefu maalum na viongozi na wafuasi wa pote hili. Kitabu hicho kimechapishwa na kinaitwa “al-Qawl al-Baliygh fiyt-Tahdhiyr min Jamaa´at-it-Tabliygh”.

Kuna mpakistani mmoja Muhammad Aslam (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kuhusu wao. Ni miongoni mwa waliotakharuji katika chuo kikuu cha Kiislamu al-Madiynah an-Nabawiyyah.

Shaykh Muhammad Taqiyy-ud-Diyn al-Hilaaliy (Rahimahu Allaah) ameandika kuhusu wao katika kitabu chake “as-Siraaj al-Muniyr fiy Tanbiyh Jamaa´at-it-Tabliygh min Akhtwaa-ihim”. Kitabu kimeingia kina zaidi kuhusu Jamaa´at-ut-Tabliygh. Kimetoa maelezo kuhusu kitabu cha Muhammad Aslam.

Jambo lao limefichuka kwa wengi miongoni mwa wale ambao walikuwa wamedanganyika nao ambapo [baadaye] wakawasusa na kutahadharisha nao. Inatosheleza kuwakemea kule kutojali kwao kulingania katika Tawhiyd. Bali uhakika wa mambo ni kwamba wanakimbiza watu na Tawhiyd na wale wenye kulingania katika Tawhiyd.

Kwa wale ambao wamedanganyika na pote hili la ki-Suufiy lililojificha na kutoka nao aambiwe kugawanywe kwa mfano “Kitaab-ut-Tawhiyd” cha Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) wakati wa kutoka kwao kisha utazame itikio lao na jinsi tabia yao nzuri itakavyogeuka kuwa unyama na ushenzi na urafiki kugeuka kuwa chuki na uadui. Haya yametokea. Hivyo utaona sura yao ya kweli.

Muftiy wa Saudi Arabia aliyetangulia na mkuu wa mahakimu na wa mambo ya Kiislamu Shaykh Muhammad bin Ibraahiym Aal ash-Shaykh (Rahimahu Allaah) amesema:

“Hakuna kheri yoyote ndani ya jumuiya hii. Ni jumuiya ya Bid´ah na upotevu. Baada ya kuvisoma vijitabu vilivyoambatanishwa, tumekuta vina upotevu, Bid´ah na propaganda za kuyaabudia makaburi na shirki, jambo ambalo haliwezi kunyamaziwa.

Hivyo basi – Allaah akitaka – tutalikemea na kufichua upotofu wake na kuraddi batili zake.” (Majmuu´-ul-Fataawaa war-Rasaa-il (01/267))

Muftiy wa Saudi Arabia aliyetangulia Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

“Jamaa´at-ut-Tabliygh hawana utambuzi juu ya ´Aqiydah. Hivyo basi, haijuzu kutoka nao ikiwa mtu hana elimu na utambuzi wa ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ili mtu aweze kuwanasihi na kuwaelekeza na kushirikiana katika wema.” (ad-Da´wah (1438) (1414-11-03)).

Amesema wakati alipoulizwa kama wanaingia ndani ya yale mapote sabini:

“Ndio, wanaingia katika mapote sabini na mbili. Yule mwenye kwenda kinyume na ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah basi anaingia katika mapote sabini na mbili.” (as-Salafiyyah (07/47) (1422)).

´Allaamah na Shams Muhaddith Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Jamaa´at-ut-Tabliygh haikujengwa juu ya mfumo wa Qur-aan, Sunnah na yale waliyokuwemo juu yake Salaf. Hivyo basi, haijuzu kutoka nao… ” (al-Fataawaa al-Imaaraatiyyah).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 32-35
  • Imechapishwa: 08/04/2017