11. Vipi mnathubutu kutahadharisha Jamaa´at-ut-Tabliygh?


Swali 11: Kwa mfano Jamaa´at-ut-Tabliygh wanasema kuwa wanataka kufuata mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na inaweza kutokea baadhi yao wakakosea. Hivyo wanauliza ni vipi mnaweza kuwahukumu na kutahadharisha juu yetu?

Jibu: Watu waliotoka na Jamaa´at-ut-Tabliygh na kusoma nao wameandika kuhusu wao. Wameandika mengi kuhusu wao na makosa kwa undani waliyotumbukia ndani. Someni vitabu vilivyoandikwa kuhusu wao ili muweze kubainikiwa na suala hili[1].

Himdi zote ni za Allaah kwa sababu Ametupa vingi vya kutosheleza na kutokuwa na haja ya kumfuata fulani na fulani. Sisi tuna mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ambao tumeshikamana nao. Hatuna haja ya Jamaa´at-ut-Tabliygh wala mwingine yeyote. Hatuihitajii.

Inapokuja kuhusiana na uhakika jinsi walivo basi kumeandikwa vitabu vingi kuhusu wao. Visomeni ili mjue. Walioandika kuhusu wao ni watu waliotoka nao, wakasafiri nao, wakachanganyika nao na hivyo wakawa wameandika kuhusu wao kwa ujuzi na ubainifu.

[1] Miongoni mwa watu walioandika kuhusu Jamaa´at-ut-Tabliygh na kufanya vizuri, kunufaisha na kuweka wazi fikira zao ni muheshimiwa Shaykh Sa´d bin ´Abdir-Rahmaan al-Husayyin kwenye kitabu “Haqiyqat-ud-Da´wah ilaa Allaah (Ta´ala)” kilichotolewa chini ya uoni wa Shaykh Faalih bin Naafi´ al-Harbiy. Amesema wakati alipoingia kwenye maana ya laa ilaaha illa Allaah kwa mujibu wa Jamaa´at-ut-Tabliygh:

“Maana yake ni kuondosha yakini ya vitu fasidi kutoka kwenye moyo na badala yake kuingiza yakini sahihi kuhusu dhati ya Allaah na kwamba hakuna muumbaji yeyote isipokuwa Allaah, hakuna mwenye kuruzuku yeyote isipokuwa Allaah na hakuna mwenye kuyaendesha mambo isipokuwa Allaah. Hili kwa hakika hakuna jengine zaidi ya Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah ambayo ilikuwa inakubaliwa na washirikina wa zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Pamoja na hivyo hawakuwa Waislamu.” (Uk. 70)

Amesema pia:

“Fikira zao ni kwamba wao ni Ahnaaf katika Fiqh, Ash´ariyyah na Maaturiydiyyah katika ´Aqiydah na Jishtiyyah, Naqshbandiyyah, Qaadiriyyah na Sahrawardiyyah katika Taswawwuf.” (Uk. 80)

Vilevile Shaykh Hamuud bin ´Abdillaah at-Tuwayjiriy (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu pekee kuhusu wao. Kitabu chake kimeingia kwa undani zaidi kuhusu pote hili. Kitabu kimeweka wazi uhakika wao uliotolewa kutoka kwenye vitabu vyao. Makosa yao yameraddiwa humo. Ukiongezea juu ya hilo ni kwamba amenukuu mashahidi wa kuaminika ambao wana uzowefu maalum na viongozi na wafuasi wa pote hili. Kitabu hicho kimechapishwa na kinaitwa “al-Qawl al-Baliygh fiyt-Tahdiyr min Jamaa´at-it-Tabliygh”.

Hata mpakistani mmoja Muhammad Aslam (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kuhusu wao. Ni miongoni mwa waliotakharuji kwenye chuo kikuu cha Kiislamu al-Madiynah an-Nabawiyyah.

Shaykh Muhammad Taqiyy-ud-Diyn al-Hilaaliy (Rahimahu Allaah) ameandika kuhusu wao kwenye kitabu chake “as-Siraaj al-Muniyr fiy Tanbiyh Jamaa´at-it-Tabliygh min Akhtwaa-ihim”. Kitabu kimeingia kwa undani zaidi kuhusu Jamaa´at-ut-Tabliygh. Kimetoa ufafanuzi wa kitabu cha Muhammad Aslam.

Sura yao ya kikweli imewabainikia wengi miongoni mwa wale ambao walikuwa wamedanganyika nao ambapo [baadae] wakawasusa na kutahadharisha nao. Inatosheleza kuwakemea kule kutojali kwao kulingania katika Tawhiyd. Bali uhakika wa mambo ni kwamba wanakimbiza watu na Tawhiyd na wale wenye kulingania katika Tawhiyd.

Kwa wale ambao wamedanganyika na pote hili la ki-Suufiy lililojificha na kutoka nao aambiwe kugawanywe kwa mfano “Kitaab-ut-Tawhiyd” cha Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) wakati wa kutoka kwao kisha utazame itikio lao na jinsi tabia yao nzuri itakavyogeuka kuwa mbaya [kama] ya unyama pori na wema kuwa chuki na uadui. Haya yamepitika. Hivyo utaona sura yao ya kikweli.

Muftiy wa Saudi Arabia alotangulia na kichwa cha maqaadhiy na wa mambo ya Kiislamu Shaykh Muhammad bin Ibraahiym Aal ash-Shaykh (Rahimahu Allaah) amesema:

“Hakuna kheri yoyote kwenye jumuiya hii. Ni jumuiya ilio na Bid´ah na upotevu. Baada ya kusoma vijitabu vilivyoambatanishwa, tumekuta vina upotevu, Bid´ah na propaganda za kuabudu makaburi na shirki, jambo ambalo haliwezi kunyamaziwa.

Hivyo basi – Allaah Akitaka – tutalikemea na kufichua upotevu wake na kuraddi batili zake.” (Majmuu´-ul-Fataawaa war-Rasaa-il (01/267))

Muftiy wa Saudi Arabia alotangulia Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

“Jamaa´at-ut-Tabliygh hawana umaizi katika ´Aqiydah. Haijuzu kutoka nao ikiwa mtu hana elimu na umaizi wa ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ili mtu aweze kuwanasihi na kuwaelekeza na kushirikiana katika wema.” (ad-Da´wah (1438) (1414-11-03)).

Amesema pidni alipoulizwa kama wanaingia katika mapote sabini na mbili [yatayoingia Motoni]:

“Ndio, wanaingia katika mapote sabini na mbili. Mwenye kwenda kinyume na ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah anaingia katika mapote sabini na mbili.” (as-Salafiyyah (07/47) (1422)).

´Allaamah na Shams Muhaddith Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Jamaa´at-ut-Tabliygh haikujengwa juu ya mfumo wa Qur-aan, Sunnah na Salaf. Hivyo haijuzu kutoka nao… ” (al-Fataawaa al-Imaaraatiyyah).

 

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Adjwibah al-Mufiydah ´an As'ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 32-35
  • Imechapishwa: 08/04/2017