Msafiri afungue kipindi cha safari yake au hapana? Hadiyth hizi zimejulisha kuwa afungue. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitoka Madiynah akiwa amefunga na wakati alipofika Kuraa´-ul-Ghamiym akafungua. Sababu ya kufungua kwake ni kuwa kuwa alifikiwa na khabari kwamba wako watu ambao swawm imekuwa ngumu kwao na kwamba wanasubiri waone kile utachofanya ili wakuige. Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa amekaa juu ya ngamia wake, akaomba chombo cha maji na akanywa baada ya ´Aswr na huku watu wanamwangalia. Alikunywa muda karibu kabla ya jua kuzama. Kadhalika wakaanya hivo wengi wao isipokuwa wachache katika wao. Dhahiri ni kwamba waliona kuwa muda uliobaki ni mdogo na wakapendelea kuendelea kumalizia funga yao. Baadaye akapashwa khabari (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba baadhi ya watu wamefunga ambapo akasema:

“Hao ni waasi. Hao ni waasi.”

Kwa sababu hawakukubali ruhusa ya Allaah pamoja na uzito.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mukhtaswar ´alaa Buluugh-il-Maraam (2/418-419)
  • Imechapishwa: 24/04/2020