Swali 11: Daktari akimjibu mgonjwa ni fatwa ipi ambayo daktari anatakiwa kuchukua au ni lazima kwa mgonjwa kurudi kwa mwanachuoni juu ya hilo?

Jibu: Ni lazima kwa mgonjwa kurudi kwa wanachuoni kuhusu yale anayoambiwa na madaktari katika hukumu za Kihari´ah. Kwa sababu madaktari wanazungumza kwa mujibu wa elimu yao. Elimu ya Shari´ah ina watu wake. Hivyo mgonjwa asitendee kazi yale anayojibiwa na daktari isipokuwa baada ya kuwarejelea wanachuoni japo kwa simu au amtume mtu amuulizie. Daktari na mtu mwingine haifai kwao kutoa fatwa isipokuwa kwa elimu. Anaweza kunukuu yale aliyowasikia wanachuoni wakisema juu ya mambo mbalimbali. Daktari anatakiwa awaulize wanachuoni mahali popote pale, kwenye hospitali yoyote ile au katika nchi yoyote ile. Ni lazima kwake kuwauliza wanachuoni wa nchi yake na maqaadhiy juu ya mambo yanayomtatiza ili ajue cha kuwajibu wagonjwa. Ni lazima kwa daktari kuuliza na hana haki ya kutoa fatwa pasi na elimu. Kwa sababu yeye sio msomi wa Shari´ah. Kazi yake yeye ajibu yanayohusiana na matibabu na achunge katika hilo na anasihi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Mariydhw, uk. 33
  • Imechapishwa: 21/05/2019