Kwa haya linapata kufahamika kosa la manaswara pale wanapojiita “wakristo” (المسيحية), kubainika kwa upotofu wake na kwamba ni dini iliyogeuzwa na kubadilishwa. Kisha baadaye Allaah akaifuta kwa kumtuma Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Shari´ah Yake ni lazima kwa waislamu. Kwani ukristo haukubaki ni dini yenye kusilihi; si kwetu sisi wala wengineo. Bali dini sahihi kwa waislamu na wengineo ni Uislamu ambao Allaah amemtumiliza kwao Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Waislamu wameamrishwa kuita katika dini yao na kuitetea. Vilevile waislamu ni wenye kupewa udhuru juu ya kubainisha upotofu wa dini zote kukiwemo mayahudi, manaswara na nyenginezo mbali na Uislamu. Kwa kufanya hivo wanakuwa wamelingania katika haki na katika Pepo na wengineo wanaita kuelekea Motoni. Allaah (Subhaanah) amesema wakati alipokataza kuwaoa wanawake wa kishirikina na kuwaoza washirikina kwa wanawake wa Kiislamu:

أُولَـٰئِكَ يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَى الْجَنَّةِ وَالْمَغْفِرَةِ بِإِذْنِهِ

“… hao wanaitia katika Moto na Allaah anaitia katika Pepo na msamaha kwa idhini Yake.”[1]

Allaah anaita kuelekea Peponi, masamaha na kuyafanyia kazi mambo hayo. Hali kadhalika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vivyo hivyo waislamu wenye kuitambua dini yake wanalingania kwayo juu ya utambuzi. Ama makafiri wengineo wanaita kwenda Motoni. Wanafanya hivo kwenye vitabu vyao, majira na vyombo vya mawasiliano.

Kwa haya inapata kufahamika kuwa haijuzu kusema kwa kuachia kwamba Uislamu na ukristo ni dini mbili zilizoteremshwa. Kwani ukristo haukubaki ni dini iliyoteremshwa. Bali imegeuzwa na kupotoshwa. Isitoshe ile haki iliyobaki imefutwa pindi Allaah alipomtumiliza Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika uongofu na dini ya haki.

[1] 02:221

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/articles/78/الاسلام-هو-دين-الله-ليس-له-دين-سواه
  • Imechapishwa: 07/10/2021