Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

6- Yeye ni wa kale asiyekuwa na mwanzo, wa daima asiyekuwa na mwisho.

MAELEZO

Amesema (Ta´ala):

هُوَ الْأَوَّلُ وَالْآخِرُ وَالظَّاهِرُ

“Yeye ndiye wa Mwanzo na wa Mwisho na Aliye juu.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wewe ndiye wa Kwanza; hakuna kabla yako kitu. Wewe ndiye wa Mwisho; hakuna baada yako kitu.”[2]

Lakini neno “wa kale” (القديم) halitumiwi kwa Allaah (´Azza wa Jall) isipokuwa kwa njia ya kuelezea. Ama kwa njia ya jina haitwi hivo. Anaitwa wa Kwanza (الأول). Wa kwanza haina maana ya wa kale. Kwa sababu cha kale kinaweza kutanguliwa kabla yake na chengine tofauti na wa kwanza ambaye hakutanguliwa na chochote.  Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Wewe ndiye wa Kwanza; hakuna kabla yako kitu.”

Hata hivyo mwandishi (Rahimahu Allaah) ametumia njia salama zaidi na akasema:

“Yeye ni wa kale asiyekuwa na mwanzo.”

Hata hivyo maana isingekuwa sahihi iwapo angelisema (القديم) kwa njia isiyofungamana.

[1] 57:03

[2] Muslim (2713).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 35
  • Imechapishwa: 13/06/2019