3- Allaah ameraddi fikira zote hizi za batili kwa yafuatayo:

a) Amewaraddi waabudu masanamu kwa kusema:

أَفَرَأَيْتُمُ اللَّاتَ وَالْعُزَّىٰ وَمَنَاةَ الثَّالِثَةَ الْأُخْرَىٰ

”Je, mmeona al-Laat na al-‘Uzzaa na Manaat, mwengine wa tatu [mliokuwa mkiwaabudu]?”[1]

Maana ya Aayah, kama alivosema al-Qurtwubiy, je, mnaona waungu hawa wamenufaisha au kudhuru mpaka wawe ni washirika wa Allaah? Je, yalijitetea nafsi zao wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake walipoyashambulia na kuyavunja[2]? Amesema (Ta´ala):

وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ إِبْرَاهِيمَ إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ مَا تَعْبُدُونَ قَالُوا نَعْبُدُ أَصْنَامًا فَنَظَلُّ لَهَا عَاكِفِينَ قَالَ هَلْ يَسْمَعُونَكُمْ إِذْ تَدْعُونَ أَوْ يَنفَعُونَكُمْ أَوْ يَضُرُّونَ قَالُوا بَلْ وَجَدْنَا آبَاءَنَا كَذَٰلِكَ يَفْعَلُونَ

“Wasomee khabari za Ibraahiym alipomwambia baba yake na watu wake: “Mnaabudu nini?” Wakasema: “Tunaabudu masanamu na tutaendelea kubaki hapo kwa kuyaabud.” Akasema: “Je, yanakusikieni mnapoyaomba au yanakunufaisheni au yanakudhuruni?” Wakasema: “Tumewakuta baba zetu wakifanya hivyo.”[3]

Wamekubali kwamba masanamu haya hayasikiii wito na hayanufaishi na kudhuru. Wanayaabudu kwa ajili ya kuwafuata kichwa mchunga baba zao. Kufuata kichwa mchunga ni hoja batili.

b) Amewaraddi wale wenye kuabudu nyota, jua na mwezi kwa kusema:

وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ وَالنُّجُومَ مُسَخَّرَاتٍ بِأَمْرِهِ

“[Ameumba] jua na mwezi na nyota – [vyote] vimetiishwa kwa amri Yake.”[4]

وَمِنْ آيَاتِهِ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ ۚ لَا تَسْجُدُوا لِلشَّمْسِ وَلَا لِلْقَمَرِ وَاسْجُدُوا لِلَّـهِ الَّذِي خَلَقَهُنَّ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ

”Miongoni mwa alama Zake ni usiku na mchana na jua na mwezi; msisujudie jua wala mwezi bali msujudieni Allaah ambaye ameviumba ikiwa Yeye pekee mnamwabudu.”[5]

c) Amewaraddi wale wenye kuwaabudu Malaika na al-Masiyh (´alayhis-Salaam) – kutokana na kwamba ni mwana wa Allaah – kwa kusema:

مَا اتَّخَذَ اللَّـهُ مِن وَلَدٍ

“Allaah hakujifanyia mwana yeyote.”[6]

بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُ وَلَدٌ وَلَمْ تَكُن لَّهُ صَاحِبَةٌ

“Mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Iweje kuwa Yeye ana mwana na hali hana mke!”[7]

لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ

”Hakuzaa na wala hakuzaliwa na wala haiwi awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye.”[8]

[1] 53:19-20

[2] Tafsiyr ya al-Qurtwubiy (20/27).

[3] 26:69-74

[4] 07:54

[5] 41:37

[6] 23:91

[7] 06:101

[8] 112:03-04

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 29
  • Imechapishwa: 29/01/2020