11. Qur-aan ndio maisha ya watu


Allaah (Ta´ala) amesema:

هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ

“… ili iwe mwongozo kwa watu na hoja bayana za mwongozo na pambanuo la batili.”[1]

Qur-aan ni mwongozo ambao Allaah amewapa watu:

وَبَيِّنَاتٍ

“… na hoja bayana… “

Ndani yake Allaah amebainisha yaliyokuwepo na yatayokuwepo. Katu tusingelijua namna alivyoumbwa Aadam endapo Allaah asingetujuza kuhusu hilo. Katu tusingelijua kuwa ´Arshi ya Mwingi wa huruma iko juu ya maji kabla ya kuumbwa mbingu na ardhi iwapo Allaah asingetujuza kuhusu hilo. Katu tusingelijua kuwa Nuuh (´alayhis-Salaam) ndiye alikuwa Mtume wa kwanza, kwamba aliwalingania watu wake miaka 950 na kwamba watu wake waliangamizwa kwa kuzamishwa endapo Allaah asingetujuza kuhusu hilo na mengineyo ya kale vilevile yaliyotajwa.

Vivyo hivyo inahusiana na yale yaliyoko huko mbele ya kwamba ardhi itabadilishwa, kusimama kwa Saa, ufufuliwaji, Qiyaamah, hesabu, Njia, neema za wachaji Allaah Peponi na adhabu ya Moto ya makafiri na wanafiki. Yote haya yamebainishwa na Allaah (´Azza wa Jall) katika Qur-aan hii.

[1] 02:185

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tafsiyr Aayaat-is-Swiyaam, uk. 22-23
  • Imechapishwa: 02/06/2017