11. Njia ya nne: mwanafunzi anatakiwa kuwa na malengo ya wazi

Miongoni mwa njia za kuipata elimu ni kuwa na malengo ya wazi na kupita njia sahihi. Mwanafunzi! Ni lazima malengo yako ya kutafuta elimu yawe wazi na ujue ni kipi unachotaka katika kujifunza elimu.

Wanafunzi wengi leo ukiwauliza wanachotaka na wanacholenga kwa kujifunza elimu, basi watajibu kuwa hawajui. Wanasema kuwa wao ni wanafunzi tu na wanachotaka ni thawabu za Allaah (´Azza wa Jall). Kuhusu lengo lake la kutafuta elimu halijamkuwia wazi. Kwa ajili hiyo utamuona anatangatanga katika kila njia na kila wiki utamuona na kitabu na kila mwezi na fani. Hatulii juu ya elimu moja, mwalimu mmoja na fani moja. Matokeo yake utamuona hafikii chochote. Alichonacho ni kama ndege; kitu kichache tu kisichokuwa na faida yoyote. Sababu ya hilo ni kutokuwa na malengo yaliyo wazi.

Mwanafunzi anapotaka kuanza kutafuta elimu anatakiwa kuwa na malengo na kusema “Mimi katika wakati na muda huu nataka nijifunze kitabu na elimu fulani”. Ajiwekee kitu anachopita kwa mujibu wake kilicho wazi. Kwa kitu hicho ataweza kupita mapito sahihi. Kwa njia hiyo atakusanya mambo mengi.

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliymillaah ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Ilm wa Wasaaailuh wa Thimaaruh
  • Imechapishwa: 22/10/2016