11. Ndio maana Mola wetu akawa ni mwenye kuzungumza tofauti na mungu wa Jahmiyyah

Ambaye hazungumzi hawezi kuwa mungu. Amesea:

وَاتَّخَذَ قَوْمُ مُوسَىٰ مِن بَعْدِهِ مِنْ حُلِيِّهِمْ عِجْلًا جَسَدًا لَّهُ خُوَارٌ ۚ أَلَمْ يَرَوْا أَنَّهُ لَا يُكَلِّمُهُمْ وَلَا يَهْدِيهِمْ سَبِيلًا

“Baada yake walimfanya ndama kutokana na mapambo yao kiwiliwili tu kilichokuwa na sauti. Je, hawakuona kuwa hawazungumzishi wala hawaongoi njia?” (07:148)

Ni dalili yenye kuonesha kuwa asiyeongea hawezi kuwa mungu. Jahmiyyah wanasema kuwa Allaah hazungumzi. Hivyo hawezi kuwa mungu. Ametakasika Allaah na yale wanayoyasema. Katika Suurah “Twaaha”:

أَفَلَا يَرَوْنَ أَلَّا يَرْجِعُ إِلَيْهِمْ قَوْلًا وَلَا يَمْلِكُ لَهُمْ ضَرًّا وَلَا نَفْعًا

“Je, hawaoni kuwa hawarudishii neno na wala hawamiliki kuwadhuru na wala kuwanufaisha?” (20:89)

Bi maana ndama.

Kwa msemo mwingine ni kwamba wanapomzungumzisha hawajibu kitu. Hawezi kuwajibu. Huyu kweli anastahiki kuwa mungu? Ibraahiym (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) alisema kuwaambia waabudu masanamu:

فَاسْأَلُوهُمْ إِن كَانُوا يَنطِقُونَ

“Waulizeni ikiwa kweli wanaweza kuongea.” (21:63)

لَقَدْ عَلِمْتَ مَا هَـٰؤُلَاءِ يَنطِقُونَ

 “Umekwishajua kuwa hawa hawaongei.” (21:63)

 أَفَتَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُكُمْ شَيْئًا وَلَا يَضُرُّكُمْ  أُفٍّ لَّكُمْ وَلِمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ ۖ أَفَلَا تَعْقِلُونَ

 “Je, mnaabudu badala ya Allaah miungu isiyokufaeni kitu chochote na wala haikudhuruni? Ole wenu kwa vile mnavyoviabudu badala ya Allaah. Kwa nini hamtii akilini?” (21:66-67)

 Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ

“Mola wenu amesema: “Niombeni nitakuitikieni.”” (40:60)

Amejisifu Mwenyewe ya kwamba anasema na kuzungumza. Ambaye hazungumzi hawezi kuwa mungu. Kwa ajili hiyo ndio maana wengi katika maimamu wamewakufurisha Jahmiyyah isipokuwa wale wanaowafuata kichwa mchunga na wafuasi wao ambao hawajabainikiwa na haki. Wamewafuata kwa ujinga. Watu hawa wanatakiwa kuangaliwa. Ni lazima kuwawekea mambo wazi. Wakiendelea baada ya hapo wanakufurishwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Sharh-is-Sunnah, uk. 21-22
  • Imechapishwa: 18/10/2017