11. Namna wasomi wengi wasivyojua msingi wa kuwasikiliza na kuwatii viongozi

Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimhu Allaah) amesema:

Kisha ikawa msingi huu haujulikana kwa wengi wenye kudai elimu. Vipi basi wataufanyia kazi?

MAELEZO

Msingi huu ikawa haujulikana kwa wengi wenye kudai elimu. Hawajui masuala ya usikivu na utiifu na umuhimu na ubora ulionayo. Tusemeje kwa wale wasiokuwa wasomi? Wao ndio wajinga zaidi kutoyajua haya. Kwa mtazamo wao ikawa mtu shujaa anayeamrisha mema na kukataza maovu na ambaye kwa ajili ya Allaah hajali lawama za wenye kulaumu ni yule ambaye anamfanyia uasi kiongozi wa waislamu na kujivua katika utiifu wake na kuita watu kuwafanyia mapinduzi viongozi wa waislamu kwa sababu wamefanya kosa au maasi yasiyofikia kiwango cha kufuru. Ikawa maongezi ya kwenye vikao, semina na mihadhara ni kufuatilia kasoro za watawala na kuzieneza na kuzichochea mpaka mambo yakafikia kutofautisha umoja [wa waislamu] na kuwafanya raia kutomtii mtawala ambapo matokeo yake amani ikakosekana na damu kumwagika. Mambo yanapelekea kupatikana uharibifu mkubwa kuliko uharibifu unaopatikana katika kuwa na subira katika kumtii mtawala ambaye ni mtenda madhambi na dhuluma anayofanya muda wa kuwa hajafanya kufuru ya wazi kabisa ambayo wana dalili kwayo kutoka kwa Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sittah, uk. 28
  • Imechapishwa: 18/05/2021