1- Ulimi ukiwa mzuri, basi viungo vyote vinakuwa vizuri. Ukiharibika, viungo pia huharibika.

2- Yahyaa bin Abiy Kathiyr amesema:

“Mtu hazungumzi vizuri isipokuwa kunaonekana kwenye matendo yake.”

3- Ibn Mas´uud amesema:

“Ninaapa kwa Allaah ya kwamba hakuna kitu kinachostahiki kutiwa jela kwa muda mrefu kama ulimi.”

5- Aliye na busara anahakikisha anaihifadhi hali yake ili isitumbukii katika makosa. Katika makosa yanayoiharibu sifa ya ndani na roho nzuri ni kupindukia katika maneno. Haya haya kama inaruhusiwa kuzungumza sana. Mtu hawezi kutilia uzito kunyamaza endapo hatoacha maneno yenye kuruhusiwa.

6- Ibraahiym at-Taymiy amesema:

“Mtu aliyesuhubiana na ar-Rabi´y bin Khaytham kwa miaka ishirini amenieleza kuwa hakupatapo kumsikia akisema kitu chenye kulaumika.”

7- Ni wajibu kwa aliye na busara kuifanyisha mazoezi nafsi yake juu ya kuacha kuzungumza maneno yenye kuruhusu ili asitumbukie katika makosa na ili kifo chake kisije kuwa yale yenye kutoka mdomoni mwake.

8- Mtu akikithirisha kuzungumza kunamfanya anaanza kupenda kuasi. Mtu asipowafikishwa kuongea yale yenye kumnufaisha Aakhirah, ni bora kwake akaacha kusema vibaya.

9- Muwarriq al-´Ijliy amesema:

“Kuna kitu ninachokitafuta kwa miaka ishirini na ambacho nitaendelea kukitafuta; kunyamazia yale yasiyonihusu!”

10- Khaarijah amesema:

“Nilisuhubiana na ´Abdullaah bin ´Awn kwa miaka kumi na tano na sidhani kama Malaika wanaandika kitu dhidi yake.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Hibbaan al-Bustiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Rawdhat-ul-´Uqalaa’ wa Nuzhat-ul-Fudhwalaa’, uk. 47-51
  • Imechapishwa: 12/11/2016