Miongoni mwa mambo ambayo yanatakiwa kutambulika ni kwamba si sharti kwa yule anayelingania katika dini ya Allaah azijue hukumu zote za dini. Lakini kilicho cha wajibu kwake ni yeye awe ni mtambuzi wa yale anayoyalingania. Kwa msemo mwingine ni kwamba awe anajua kwa mujibu wa elimu ya dini yale masuala ambayo anawalingania watu kwayo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) amesema:

“Fikisheni kutoka kwangu ijapo Aayah.”[1]

Hivyo muislamu akiitambua Aayah, Hadiyth au hukumu na akafahamu maana yake kupitia kwa wanachuoni na wafasiri na vitabu vya wanachuoni vilivyotungwa, basi anatakiwa kuwafikishia watu wengine. Haijalishi kitu hata kama hajui si mtambuzi wa hukumu, Hadiyth au Aayah nyenginezo.

Shaykh na ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Qaasim (Rahimahu Allaah) amesema katika maelezo yake ya chini ya “Kitaab-ut-Tawhiyd”:

“Kulingania katika dini ya Allaah ni lazima kupatikane sharti mbili:

1- Ulinganizi wake uwe umetakaswa kwa ajili ya kutafuta uso wa Allaah.

2- Ulinganizi wake uafikiane na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam).

Jengine ni kwamba mlinganizi awe ni mtambuzi wa yale anayoyalingania.

Akiharibu sharti ya kwanza basi atakuwa mshirikina. Akiharibu sharti ya pili basi atakuwa mzushi… “[2]

[1] al-Bukhaariy (3461).

[2] Uk. 55.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Usuwl-ud-Da´wah as-Salafiyyah, uk. 37-38
  • Imechapishwa: 05/08/2020