4- Mimba na kunyonyesha. Mwanamke akiwa mjamzito au mnyonyeshaji na akachelea juu ya nafsi yake au mtoto wake kwa sababu ya funga hiyo, basi inafaa kwao kula. Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amepokea kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah amemwondoshea msafiri nusu ya swalah na swawm kwa msafiri, mjamzito na mnyonyeshaji.”[1]

Mjamzito na mnyonyeshaji watalipa idadi ya zile siku walizokula. Hapo ni pale ambapo watachelea juu ya nafsi zao. Pamoja na hilo mjamzito akichelea juu ya kipomoko chake au mnyonyeshaji juu ya yule mtoto anayemnyonyesha, basi watalipa pamoja na kulisha kwa kila siku moja masikini. Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Mnyonyeshaji na mjamzito wakichelea juu ya watoto wao basi watafungua na kulisha.”[2]

Kwa hiyo tunafupiza kutokana na hayo kwamba sababu zinazojuzisha kula ni nne:

1- Safari.

2- Ugonjwa.

3- Hedhi na damu ya nifasi.

4- Kuchelea kufa, kama ilivyo kwa mjamzito na mnyonyeshaji.

[1] at-Tirmidhiy (715) ambaye ameifanya kuwa nzuri, an-Nasaa´iy (02/103), Ibn Maajah (1667). Ni nzuri pia kwa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan-in-Nasaa´iy” (2145).

[2] Abu Daawuud(2317, 2318). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Irwaa´” (04/18,25). Imepokelewa mfano wake kutoka kwa Ibn ´Umar.

  • Mhusika: Nukhbatin minal-´Ulamaa´
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fiqh-ul-Muyassar, uk. 156-57
  • Imechapishwa: 23/04/2020