11. Mfungaji akate swawm akifika katika mji usiofunga?


Swali 11: Kuna mtu yuko katika mji wake pindi ilipoingia Ramadhaan. Baada ya hapo akasafiri kwenda katika nchi ya jirani na kukuta wakazi wa mji huo hawajaanza kufunga. Nia yake ni kubaki katika nchi hiyo zaidi ya siku nne. Je, aache kufunga?

Jibu: Akifika katika nchi hiyo iliyo jirani na akakuta kuwa hawafungi ilihali yeye amefunga, aendelee kufunga kwa kuwa atarudi katika mji wake. Aendelee kufunga. Ama ikiwa atabaki katika nchi hiyo ya jirani ana hukumu moja kama wakazi ya kuacha kufunga.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 26
  • Imechapishwa: 12/06/2017