11. Mfano wa sita kuonyesha jinsi Raafidhwah wanavodai kuwa Maswahabah wamepotosha Qur-aan


al-Kulayniy amesema katika “al-Kaafiy”[1]:

“Wengi katika watu wetu waaminifu wamepokea kutoka kwa Sahl bin Ziyaad, ´Aliy bin Ibraahiym na baba yake, kutoka kwa Ibn Mahbuub, kutoka kwa Hamzah bin Abiy Yahyaa, kutoka kwa al-Aswbagh bin Nabaatah ambaye ameeleza kuwa amemsikia kiongozi wa waumini akisema:

“Qur-aan imeteremka ikiwa theluthi (1/3); moja inahusu sisi na maadui zetu, nyingine inahusu watu waliotangulia na mifano na sehemu nyingine inahusu mambo ya faradhi na hukumu.”

“Iko wapi sehemu ya Tawhiyd, Mitume na ulinganizi wao na Pepo na Moto? Nini maana ya theluthi inayohusu watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na maadui zao? Kwa nini hakukutajwa fadhila za Maswahabah na kuwasifu akiwemo ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu), Abu Bakr, ´Umar na ´Uthmaan? Je, ´Aliy anapinga hilo?

Allaah Amemtakasa ´Aliy na uongo huu na kumzulia uzushi Allaah na Kitabu Chake.

[1] 02/627.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 40-41
  • Imechapishwa: 19/03/2017